Kahama
Kahama FM

KAHAMA:Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa wa mauaji na matapeli Sugu.

May 27, 2021, 4:28 pm

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wawili SHINJE NGULA (23) mkazi wa Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini na KISINZA LUSAMILA (28) mkazi wa mkoani katavi kwa kosa la mauaji ya HADIJA KISINZA mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga DEBORA MAGILIGIMBA amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kahama, ambapo amesema mnamo Tarehe 14 mwaka huu saa mbili usiku katika kijiji cha Mawemilu mkoani shinyanga lilitokea tukio hilo la mauwaji.

Sauti ya Kamanda wa Polisi akiongea na waandishi wa habari leo Mjini Kahama.

Hata hivyo, katika tukio lingine jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa watatu, DISMOND ZACHARIA(33), FEISALI HUSSENI (27) Mpemba Anbaye ni mtaalam wa Teknolojia ya mawasiliano na JUMA ALMAS (35) mfanyabiashara, baada ya kukamatwa wakiwa na nyaraka mbalimbali za kughushi kwa lengo la kutapeli wananchi.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Debora Magiligimba akiongea na waandishi wa habari.

Sambamba na hayo Jeshi la Polisi limemkamata Elina Zacharia (19) mkazi wa Kagongwa akiwa na kete za bangi zipatazo 111 akiwa nyumbani kwa Lucia Luhende ali maarufu mama Bonge ambaye ndiye mmiliki wa bangi hiyo.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga amewataka wananchi kuwa makini na mtandao huo wa matapeli,   na wameombwa kufikisha taarifa katika kituo cha polisi kilichopo karibu ili waweze kushughulikiwa haraka.