Kahama FM

Wanaume wafanyiwa ukatili na wanawake.

May 6, 2021, 7:23 pm

Imeelezwa kuwa Moja ya ukatili wa kijnsia unaojitokeza katika kata ya Nyamilangano halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga, ni baadhi ya wakina baba kupigwa na wake zao hali inayosababisha kutelekeza familia zao pamoja na wanandoa kutokugawana mali inapotokea wameachana.

Akizungumza katika kikao cha maendeleo ya kata (ODC) mtendaji wa kata ya Nyamilangano LAURENT MIHAYO amesema kuwa kumekuwepo na  ukatili wa kijinsia kwenye ndoa ambapo kunafanya watoto kuteseka, na kuwataka viongozi wa serikali ya vijiji kulishughulikia tatizo hilo ili kuondokana na changamto hiyo katika jamii.

INSERT………….LAURENT WABABA

Naye, diwani wa kata ya Nyamilangano ROBART MIHAYO amesema wanaume na wanawake waliopo kwenye ndoa wanapaswa kuheshimu na kupenda ndoa zao ili kuondokana na matatizo ikiwemo kutelekeza familia zao, ambapo amewataka wanawake kuwatii waume zao.

INSERT………ROBART WABABA

Kwa upande wao, katibu wa baraza la ushauri na mtendaji wa kijiji cha hundi wamesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kusimamia suala hilo ili kuondokana na changamoto hizo ambazo zinawaathiri watoto katika familia.

INSERT……….WAJUMBE ODC