Kahama FM

Umoja wa wanawake Tanzania wa chama cha mapinduzi (UWT) wilaya ya Kahama, umetoa msaada kwa Shule ya msingi Kahama A.

May 6, 2021, 4:32 pm

Umoja wa wanawake Tanzania wa chama cha mapinduzi (UWT) wakitoa msaada

Umoja wa wanawake Tanzania wa chama cha mapinduzi (UWT) wilaya ya Kahama, umetoa msaada kwa Shule ya msingi kahama A iliyopo katika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga  ambapo imepatiwa masinki 10 ya vyoo yenye thamani ya shilingi laki mbili ili kuendelea kupunguza changamoto ya vyoo shuleni hapo.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi masinki hayo katika shule hiyo, Mwenyekiti wa umoja huo TERESIFORA SALIA amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya watoto wapate vyoo bora pamoja na kuongeza nguvu katika vyoo hivyo ambavyo vilianza kujengwa tangu mwaka 2019.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo NEEMA ELIBARIKI amesema vyoo hivyo vilishindwa kukamilika kwa wakati kutokana kutegemea michango kutoka kwa wazazi, ambapo kupitia ofisi ya kata wamepata wadau wa kuchangia mradi huo ili uweze kukamilika na kuwashukuru uongozi wa UWT kwa kuwezesha kuwapatia masinki hayo ambayo yatapunguza gharama za mradi huo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kahama mjini HAMIDU JUMA amewashukuru wanawake wa UWT kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitakwenda kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kuwataka wadau wengine kijitokeza kuendelea kuachangia katika miradi mbalimbali ya maendeo katika kata hiyo.

Ikumbukwe mradi wa ujenzi wa vyoo hivyo ulianza tangu mwaka 2019 kwa nguvu za wananchi na wadau wa maendelea, ambapo mpaka sasa umefikia hatua nzuri kukamilika na wanafunzi kuanza kutumia vyoo hivyo.