Kahama FM

Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba bodi ya tumbaku Tanzania kushughulikia tatizo la vyama vya msingi.

May 6, 2021, 7:06 pm

Baraza la madiwani Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama

Madiwani wa Halmashauri ya ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba bodi ya tumbaku Tanzania kushughulikia tatizo la vyama vya msingi vinne ambavyo havijalipwa fedha zao tangu msimu uliopita na makapuni ya ndani ya ununuzi wa tumbaku.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira KULWA SHOTO, amesema kuwa hadi sasa vyama hivyo vinadai fedha za kidola za marekani 68,000,ambapo mpaka muda huu wa simu mpya unaanza lakini bado fedha hizo hawajaliwa.

Akitoa ufafunzi juu ya suala hilo mteuzi mkuu wa bodi ya tumbaku Tanzania ALBART CHARLES, amesema kuwa kutokana na makapuni hao kutokuwa na mitaji mikubwa pamoja kuwepo kwa ugonjwa covid-19 mwaka jana kumesababisha kukosa masoko na kushindwa kuwalipa wakulima wa tumbaku wa vyama nne vya msingi vya tumbaku katika halmashauri hiyo.

Wakati huohuo, madiwani wa kata ya Ulowa na   Nyamilangano GABIELA KIMARIO NA ROBART MIHAYA, wamesema wakulima hao wanapaswa kulipwa fedha zao pamoja na kuitaka bodi hiyo kushughulikia changamoto ya kupoteza ubora pindi ya wanaposafiriaha tumbaku kwenda katika soko lililoopo Kahama.

Hata hivyo, msimu mpya wa soko la tumbaku umeanza tangu April 28 mwaka huu na unaendelea kwa kipindi cha miezi mitatu, japokuwa kuna vyama vinne ambavyo havijalipwa vikiwemo mlinza, Ibambala, Kasandala na Isanjandugu.