Kahama FM

Vibaka 17 wakamatwa Shunu Kahama,RPC awashukia wazazi.

April 29, 2021, 9:52 am

Vibaka wakabaji 17 wenye umri chini ya miaka 18 wamekamatwa mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga manispaa ya kahama na jeshi la polisi katika oparation maalumu iliyofanyika kwa muda wasiku tatu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa jeshi la  polisi Debora Magiligimba.

Wakazi wa mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameulalamikia uongozi wa  sungusungu wa mtaa wa Shunu kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi  unaotekelezwa na makundi ya vijana wajulikanao kama panyarodi ambao wamekuwa wakivunja nyumba na kupora mali za watu nyakati za usiku.

Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa jeshi la  polisi Debora Magiligimba katika mkutano wa hadhara ulikuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wakazi hao.

Wananchi wa Mtaa wa Shuku wakitoa malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga.

Baada ya kusikiliza kero hizo kamanda Magiligimba akatoa msimamo wa jeshi la polisi kuhusiana suala la uongozi pamoja na namna hatua zilizochukuliwa katika kulidhibiti kundi hilo.

Samba na hilo kamanda Magiligimba akatoa rai kwa wazazi kuhusiana na suala la malezi kwa watoto ili kuzuia wasijiingize katika makundi hatarishi.

Sauti ya kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba.