Kahama FM

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP DEBORA MAGILIGIMBA amefanya ukaguzi kwa mabasi, Kituo Cha Mabasi Kahama.

April 25, 2021, 4:41 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP DEBORA MAGILIGIMBA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP DEBORA MAGILIGIMBA leo Jumapili Aprili 25,2021 saa 11 alfajiri amefanya ukaguzi kwa mabasi yaendayo mikoani kutoka Kituo Cha Mabasi Kahama na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria na madereva wa magari hayo.

Akiwa eneo hilo, Kamanda MAGILIGIMBA amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kuendesha mabasi  kwa mwendokasi.

Sauti ya kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP DEBORA MAGILIGIMBA

Aidha MAGILIGIMBA amewataka abiria kutoa taarifa pindi wanapobaini mienendo mibovu ya madereva wanapoendesha vyombo vya moto.

Katika hatua nyingine, MAGILIGIMBA ametoa wito kwa madereva kuendelea kuzingatia sheria za barabarani, ambapo amewataka wamiliki wa mabasi kutoruhusu  mabasi yenye hitilafu kusafirisha abiria,  huku akiahidi kuwa zoezi la ukaguzi wa magari ni zoezi endelevu katika manispaa ya Kahama.

Sauti ya kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP DEBORA MAGILIGIMBA