Kahama FM

Mkazi wa Nyasubi wilayani Kahama leo afikishwa katika Mahakama ya wilaya.

April 21, 2021, 7:15 pm

Mkazi wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga JONATHANI JULIUS MANYAMA mzanaki (32) leo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa shauri lake la ubakaji Pamoja na kumpa ujauzito mwanafunzi  wa kidato cha nne wa shule ya sekondari  Nyasubi .

Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo DAVID MSALILWA mwendesha mashtaka upande wa Jamuhuri ATHUMANI KISANGO amesema mnamo January 22  mwaka huu,eneo la Nyasubi mshtakiwa alimbaka msichana (17)katika shamba la mahindi lililopo eneo hilo ambapo muhanga wa tukio  alikuwa akipita. 

KISANGO amesema mshitakiwa  alimbaka  mwanafunzi huyo (17) wa kidato cha  nne ambapo ni kinyume cha sheria kifungu cha 130(1) na (2) ,(e) na kifungu cha 131(1) cha sheria  cha kanuni ya adhabu.

baada ya kusomewa maelezo ya awali amekubali majina  na anuani yake ya makazi lakini amekana kumbaka mlalamikaji, huku upande wa jamuhuri ukiongozwa na mwendesha mashtaka athumani kisango umesema utaleta mashahidi wanne  may 12 mwaka huu kesi  itakapoanza kusikilizwa tena ambapo mshitakiwa anaendelea na dhamana yake.