Kahama FM

Waandishi wa habari wametakiwa kuandika kwa weledi, habari zinazohusu watu wenye ulemavu.

April 15, 2021, 4:14 pm

MLEMAVU MBOGWE
Mtoto mwenye ulemavu

Waandishi wa habari mbalimbali nchini Tanzania wametakiwa kuandika na kuziwasilisha kwa weledi habari zinazohusu watu wenye ulemavu ili kupunguza unyanyapaa katika jamii.

Hayo yameelezwa leo na mkufunzi ALLY MWADINI akiwa visiwani zanzibar kwenye mafunzo yanayohusu habari za watu wenye ulemavu yaliyoandaliwa na  shirika la internews kwa njia ya mtandao.

MWADINI amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwatenga watu wenye ulemavu na kuwaona hawana maana katika jamii kitu ambacho si sahihi kwani kuna waliopo katika nyadhfa mbalimbali na wana ulemavu.

Sauti ya Mkufunzi ALLY MWADINI

Aidha ameongeza kuwa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa jamii iliyokuwa na mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari.

Mafunzo kuhusu watu wenye ulemavu kwa waandishi wa habari ni yatafanyika kwa siku tatu, ambapo yamejumuisha waandishi wa habari kutokamikoa mbalimbali ya Tanzania na yanafanyika kwa njia ya mtandao yaliyoandaliwa na shirika la Internews Tanzania.