kenya
Kahama FM

Mwandishi wa habari auwawa kwa kupigwa Risasi kichwani.

April 9, 2021, 8:32 am

Mwandishi wa habari wa Shirika la utangazaji Kenya -KBC, Betty Barasa ameuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake ambako ni pembezoni mwa mji mkuu wa Nairobi.

Mwandishi wa habari wa Shirika la utangazaji Kenya -KBC, Betty Barasa

Wanaume wawili wenye silaha waliingia nyumbani kwa Barasa wakati alipokuwa anaendesha gari akiwa anatoka kazini kwake majira ya jioni.

Walimuamuru mume wa mwandishi huyo na watoto wake kulala chini na mwanaume mmoja mwenye silaha akampeleka bi. Barasa chumbani kwake.

Baada ya muda walisikia milio ya risasi mara mbili na wanaume hao wakawa wanatoka chumbani humo.

Polisi wa eneo la Ngong wanasema bi. Barasa alikuwa na jeraha katika kichwa.Chanzo cha mauaji hayo hakijaelezwa.

Baraza la habari nchini Kenya limelaani vikali mauaji hayo na kutaka uchunguzi kuharakishwa