Kahama FM

Philip Mpango apendekezwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

March 30, 2021, 11:50 am

Waziri wa Fedha Philip Mpango

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amempendekeza Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kinachofuata sasa ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuthibitisha jina lake katika kikao cha bunge kinachoendelea muda huu jijini Dodoma.

 Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Rais SAMIA amepeleka bungeni jina la Dkt. PHILIP MPANGO ili awe Makamu wa Rais na kwamba utaratibu wa kupiga kura unafanyika bungeni.

Sauti ya Spika wa bunge Job Ndugai