Kahama FM

Wananchi Manispaa ya Kahama Wamlilia JPM,

March 28, 2021, 1:54 pm

Wakazi wa manispaa ya KAHAMA mkoani SHINYANGA wameeleza kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa raisi wa TANZANIA JOHN POMBE MAGUFULI

Hayati Dr John Pombe Magufuli

Wakizungumza na KAHAMA FM baadhi ya wakazi hao,FANUEL NZAGAMBA na SAMWELI MATIKO wamesema hayati MAGUFULI alikuwa na maono yenye matokeo chanya kwa taifa na mtetezi wa wanyonge hivyo kuondoka kwake ni pengo kubwa kwa taifa la Tanzania.

Katika hatua nyingine wamesema watamkumbuka kwa miradi mikubwa aliyoicha ikiwemo,umeme,barabara pamoja na sera ya elimu bure.

Wameongeza kuwa suala la kifo halizuiliki hivyo wamemuombea hayati JOHN POMBE MAGUFULI Apumzika kwa amani.

Wakazi wa Kahama wakiongea na KAHAMA FM.