Jamii FM

Manispaa ya Mtwara Mikindani yavuka lengo la Chanjo ya Polio

26 May 2022, 15:01 pm

Na Gregory Millanzi

Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani iliyopo Mkoani Mtwara imevuka lengo la Uchanjaji wa Chanjo ya Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano baada ya kuchanja Watoto elfu 18760 sawa na asilimia 119 Kati ya elfu 15760 waliolengwa.

Manispaa ya Mikindani imewashukuru wazazi na walezi kuwapeleka Watoto Kupata Chanjo kwenye Vituo vya kutolea Chanjo vilivyoandaliwa pamoja na kutoa ushirikiano kwa watoa huduma ambao walipita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kutoa Chanjo hiyo.

Watoto wakipata huduma ya Chanjo ya Polio kwa mtoa Huduma baada yakuwafata Shuleni.

Baadhi ya wazazi na walezi wameishukuru Serikali kwa kuwaletea kampeni hii ya Chanjo ya Polio ambayo itasaidia kuwalinda watoto na virusi hivyo.

“Naishukuru sana Serikali chini ya Rais Mama Samia kwakutuletea Chanjo ya Polio maana tumeweza kuwakinga watoto wetu, kweli mama anatujali wananchi wake, Mungu ambariki sana” amesema Zainabu Juma mkazi wa Chuno.

Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Polio ilianza Mei 18 na Kumalizika Mei 21,2022.