Jamii FM

Mwaka wa 7 hatuna maji safi na salama

21 May 2021, 04:52 am

Na Karim Faida.

Wananchi wa Kijiji cha Lyowa kata ya Muungano halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani hapa, wameiomba serikali kupitia Wakala wa usambazaji maji na usafi wa masingira RUWASA, kuwarekebishia mradi wao wa maji maarufu kama Mradi wa maji Mpapura – Lyowa uliokuwepo tangu 2014.

Ndugu Ismaili Bashehe, Mkazi wa Lyowa

Akiongea na Jamii fm radio Ndugu Ismaili Bishehe mkazi wa kijiji hicho amesema kuna tenki limejengwa kijijini hapo lakini halina kazi yoyote kwa kuwa maji hayajazwi kwenye tenki hilo huku akisema mradi huo ni wa muda mrefu na wao hawajafaidika nao na hivyo kuendelea kunywa maji ya kuokota yanayotumiwa pia na wanyama.

Omari Kayanda, Fundi sanifu RUWASA

Nae Hassani Likutwe, Mkazi wa kijiji hicho amesema kutokana na busta iliyofungwa kwenye kijiji cha Nanyani ina nguvu hali inayopelekea mabomba kupasuka mara kwa mara na hivyo amewaomba TARURA kubadilisha mabomba hayo katika maeneo fulani ili kuhimili msukumo wa maji na yaweze kufika Lyowa.

Mwenyekiti wa kijiji cha Lyowa Ndugu Hassani Mmanda amekili kuwepo kwa shida hiyo ya maji na kupelekea wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta maji hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya Kijiji chake.

Busta iliyofungwa kijiji cha Nanyani ili kusaidia kuongeza presha ya maji

Nae Ndugu Omari Kayanda ambae ni fundi sanifu kutoka ofisi ya RUWASA, amesema kweli zipo changamoto katika mradi huo ambazo wanazifanyia na ameahidi ndani ya siku tatu wananchi wa kijiji cha Lyowa wataanza kunywa maji safi na salama.