Jamii FM

Hodi Mtwara, Brigedia Jenerali Gaguti

20 May 2021, 19:12 pm

Na Karim Faida

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewaomba wananchi wa Mtwara kumpa ushirikiano zaidi ya ule alioupata aliyekuwa mkuu wa mkoa huu Ndugu Gelasius Byakanwa.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti

Amesema hayo leo katika ukumbi wa Boma uliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara mbele ya watumishi mbalimbali wa serikali wa mkoa huu pamoja na waandishi wa habari.

aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa

Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa huu Ndugu Gelasius Byakanwa, amempongeza mkuu wa mkoa huyo mpya kwa kuteuliwa tena huku akimuomba kulisimamia swala la zao la korosho pamoja na rasilimali za Gesi na Mafuta.

Mkuu wa wilaya ya Newala Bi Aziza Mangosongo

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Newala Bi Aziza Mangosongo akiwawakilisha wakuu wa wilaya wenzake, amesema watampa ushirikiano Bregedia Gaguti ili kuhakikisha Mtwara inazidi kusonga mbele kimaendeleo.