Jamii FM

Mbae: Barabara ni changamoto

5 May 2021, 04:41 am

Na karim Faida

Wananchi wa mtaa wa Mbae Chundi, Kata ya Ufukoni manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wameiomba serikali kuwatengenezea barabara inayotoka Pacha ya Mbae hadi Mtaa wa Mbawala chini kwa kiwango cha changalawe.

Eneo korofi la Barabara- Mbae chundi

Wakiongea na Jamii fm radio baadhi ya wananchi wa mtaa huo na watumiaji wengine wa barabara hiyo wamesema uwepo wa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara ndio chanzo kikubwa cha kuharibika miundombinu mingi ya barabara hiyo na kukwamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa hupitika kwa shida.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbae Chundi Ndugu Amos Sisangu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbae Chundi Ndugu Amos Sisangu amesema ni kweli ubovu wa barabara hiyo umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya watu wa mtaa wake.

Wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA Mkoa wa Mtwara Injinia Paulo Mhele

Hata hivyo amewatoa wasiwasi wananchi hao na kusema Serikali inalitambua hilo na watalifanyia kazi.Hata hivyo Kaimu Mratibu wa Wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA Mkoa wa Mtwara Injinia Paulo Mhele amesema ni kweli barabara nyingi zimeharibika kutokana na mvua na kuahidi kuwa hadi kufika Juni 30 mwaka huu, sehemu zote korofi zitakuwa zimesharekebishwa.

Injini Mhele, amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa hawawezi kutengeneza barabara huku mvua ikiendelea kunyesha.