Jamii FM

SDA: acheni kuficha watoto walemavu

9 April 2021, 17:02 pm

Na Karim Faida

Shirika la Sports Development Aid SDA la hapa mkoani Mtwara wamewataka watu wanaowaficha watoto wenye ulemavu kuwafichua na kuwapeleka shule ili waweze kupata elimu ambayo itawasaidia baadae katika maisha ya baadae ikizingatiwa kwamba Elimu ni haki ya msingi ya mtoto.

Jackline Mpunjo ambaye ni mratibu wa Mradi wa Empowered Girls speak out

Akiongea katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya Michezo, Maendeleo, na Amani lililofanyika leo April 9 2021 katika viwanja vya shule ya Msingi Nachenjele Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Jackline Mpunjo ambaye ni mratibu wa mradi wa Empowered Girls speak out amesema lengo la tamasha hilo ni kuitaka jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Nae Bi Somoe Kijusi mkazi wa Kijiji cha Mdui ambae ni mlemavu wa Miguu amesema pale wanapoona mtoto mlemavu amefungiwa ndani wanamfuata mzazi wa mtoto huyo na Kumtaka kuacha mara moja tabia hiyo ili watu wamuone na waweze Kumpa msaada.

Some kijusi mkazi wa Nachenjele akizungumza na Jamii fm

Mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya msingi Mdui Nasri Anafi ambaye ni mlemavu wa ngozi ameshiriki tukio hilo huku akisema anatamani kuwa Daktari baada ya kumaliza masomo yake huku akisema kuwa wanafunzi wenzake wanampenda na hawajawahi kumnyanyasa kwa kuwa mlemavu.

Mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya msingi Mdui Nasri Anafi akizungumza na Jamii fm

Kwa upande wake mwenyekiti wa walemavu kijiji cha Nachenjele Akili Akili ameipongeza SDA kwa kuandaa tukio hilo kwa kuwa itasaidia kuonesha thamani ya walemavu kwa jamii na hivyo kuwaibua na kuwashikisha walemavu hao katika mambo mbalimbali ya kijamii.

mwenyekiti wa walemavu kijiji cha Nachenjele, Akili Akili

Mradi wa Empowered Girls speak out upo chini ya Shirika la Sports Development Aid SDA unatekelezwa katika wilaya sita za mkoa wa Mtwara ukiwa na lengo la kuikwamua jamii yenye uhitaji ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu.