Ileje FM

Wananchi waipongeza serikali kutatua mgogoro wa eneo la kuzika

September 12, 2023, 12:22 pm

Mmoja wa wananchi Six Msongole akizungmza kwenye mkutano kuipongeza serikali baada ya kumaliza mgogoro( Picha na Maoni Mbuba)

Na Maoni Mbuba, Songwe

Wananchi wa kijiji cha Mbebe kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani Songwe waipongeza serikali kupitia kwa mwanasheria wa halmashauri hiyo kumaliza mgogoro wa maeneo ya kuzika baina ya wananchi kijijini hapo.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo ukiongozwa na mwanasheria wa wilaya ya Ileje Casmir Msofu wakati akitoa elimu ya utengaji maeneo ya kuzika baada ya kutokea sintofahamu baina ya wananchi na ukoo wa akina Kamendu ambao walizika ndugu yao kwenye eneo lililotengwa na wana ukoo.

Wananchi hao wameeleza  kukosekana kwa elimu ya kuzika ndugu zao majumbani imesababisha mgogoro ambao haukuwa na maana.

Kwa upande wake mwanasheria huyo Casmir Msofu ametoa elimu kwa wananchi juu ya utengaji wa maeneo ya mazishi huku akisema akina kamendu walikuwa sahihi kuzika kwenye eneo lao.

Hata hivyo wananchi hao wamemtupia lawama mwanasheria huyo kuchelewa kutoa elimu hiyo.