Ileje FM

Kamanda wa polisi akanusha askari kupasuliwa fuvu la kichwa Songwe

October 19, 2021, 12:03 pm

kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Janeth Magomi amekanusha taarifa iliyosambaa kwenye vyombo vya habari juu ya baadhi ya askari wa jeshi la polisi wilayani Mbozi kupasuliwa fuvu la kichwa na wananchi wenye hasira kali wa kijiji cha Mpanda kata ya Nyimbili wilayani humo.

akizungumza na kituo hiki kamanda Magomi amesema amesekitishwa na taarifa hizo kwenye baadhi ya magazeti na kudai kuwa askari aliyejeruhiwa ni wa Suma Jkt na si askari Polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Janeth Magomi akitoa ufafanua wa tukio.

Aidha kamanda Magomi amesema upelelezi wa tukio bado unaendelea ili kujuwa nini chanzo cha tukio hilo.

sauti ya kamanda Magomi

Mmoja wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio, Mussa Mgode amedai askari hao walikuwa watatu  na  hawakuva  sare za jeshi wakiwa na pikipiki mbili walifika eneo hilo majira ya saa 9 alasiri kisha walimkamata mtu mmoja aliyedai kuwa amebeba magendo.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, George Mwambubha   amesema mara kadhaa askari hao wamekuwa wakifika kijijini hapo na kukamata vijana wanaosafirisha magendo ya mafuta ya kula na pombe za viroba kutoka Malawi.