Ileje FM

Ulaji wa kinyesi kibichi unavyosababisha vifo kwa watoto wadogo

October 13, 2021, 8:58 am

Hayo yalibainishwa na wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi mazingira na matumizi bora ya vyoo, uliozinduliwa Kimkoa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba Mjini Vwawa, Wilayani Mbozi.

Mkuu wa mkoa wa Songwe mh. Omary Mgumba akizindua kampeni ya usafi wa mazingira

Mgumba amesema Ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na ulaji wa kinyesi kibichi umetajwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa vifo vya watoto wadogo walio chini ya miaka mitano.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa jamii hususani akina mama kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kuanza kunyonyesha watoto wao.

Akizungumzia kuhusu matumizi bora ya vyoo, Mgumba amesema hadi kufikia sasa Mkoaa wa Songwe umetekeleza zoezi hilo la matumizi ya vyoo bora kwa asilimia 63 tuu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaonyesha kuwa magonjwa ya homa ya mapafu (Nimonia) na ule wa kuhara huua watoto milioni mbili kila mwaka sawa na asilimia 29 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano duniani kote.