Huheso FM

Wananchi Nyandekwa waunga juhudi za maendeleo

November 9, 2022, 10:12 am

Wananchi wa vitongoji vya kigungumli na baseka vilivyopo nyandekwa  manispaa ya kahama mkoani shinyanga  wameungana kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika maendeleo kwa kuitisha harambee yenye lengo la ujenzi wa shule ya msingi.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na watoto wanaoishi katika vijiji hivyo kutembea umbali mrefu kwenda shule hali ambayo inahatarisha usalama wao barabarani kwa kugongwa na magari.

Hayo yamesemwa na mtendaji wa kijiji cha Nyandekwa,..wakati akisoma risala iliyoandaliwa na ofisi ya serikali Mtaa kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa Wilaya ya Kahama, FESTO KISWAGA ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi amewashukuru viongozi wa serikali ya vijiji hivyo kwa kufanya jambo la msingi.

Aidha mkutano huo umeudhuriwa na wadau mbalimbali wamaendeleo akiwemo AMOSS KADONYA ambaye amechangia kiasi cha shilingi Milion 2 nanusu kwaajili ya ujenzi katika shule hiyo

Baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali wakizungumza na HUHESO FM juu ya harambee hiyo wameishukuru serikali kwa kuwaunga mkono katika ujenzi huo wa madarasa na matundu ya vyoo kwani fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa shuleni hapo.

.