Huheso FM

Wananchi Kahama watakiwa kushiriki zoezi la sensa

July 22, 2022, 11:29 am

Wananchi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti 23, 2022.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga leo Julai 21, 2022 wakati akizungumza na HUHESO fm amesema maandalizi ya zoezi la sensa kwa wilaya ya Kahama yapo vizuri ambapo wananchi wote wilayani Kahama watahesabiwa.

Amesema zoezi la uhamasishaji wananchi kushiriki zoezi la sensa linaendelea ambapo kwa sasa lipo kwenye ngazi ya familia ambapo maeneo yote ya mikusanyiko elimu ya sensa inatolewa.

Hata hivyo sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022 yenye kaulimbiu isemayo “sensa kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa”.