Huheso FM

Maafisa Manispaa ya Kahama wapatiwa pikipiki za utekelezaji majumu yao

July 6, 2022, 8:02 pm

  1. Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga imegawa jumla ya pikipiki 19 kwa Maafisa kilimo, Bibi maendeleo ya jamii  na watendaji katika Kata za Manispaa hiyo

Akizungumza baada ya zoezi la ugawaji wa pikipiki hizo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhan amesema Manispaa walitenga bajeti ya millioni 57.95 kwa ajili ya ununuzi wa Pikipiki hizo na amewataka Maafisa hao  kuzitumia vizuri kwenye maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wao Maafisa waliopokea Pikipiki hizo wameishukuru ofsi ya mkurugenzi kwani itawarahisishia kufanya kazi kutokana na changamoto walizokuwa nazo za kukosa usafiri..

Hata hivyo bajeti ya fedha iliyogaharimu kununua pikipiki hizo ni mapato ya ndani ya halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga