Huheso FM

Wananchi watakiwa kushiriki anuani za makazi

March 25, 2022, 7:17 pm

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga Clemence bernald Mkusa amewataka wananchi wilayani humo kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la anuani za makazi ili kurahisisha watoaji wa huduma ya sensa kufahamu mipango ya maendeleo katika  jamii.

Ameyasema hayo leo katika kikao cha baraza la madiwa Kichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya kahama wakati akitoa taarifa na utambulisho wa zoezi la anuani za makazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Kahama Thomas Muyanga amewataka wakuu wa idara, madiwani na wananchi wote kuliunga mkono zoezi la anuani za makazi litakalofanyika.

Hata hivyo zoezi hili la anuani za makazi ni maandalizi ya sensa  ya watu na makazi ambayo itarajiwa kufanyika hapa nchini Tanzania mnamo agosti mwaka huu.