Huheso FM

Madimbwi ya maji changamoto katika makazi ta watu

March 12, 2022, 12:21 pm

Kutokana na kuwepo kwa madimbwi ya maji kwenye maeneo ya makazi ya watu katika msimu wa huu wa mvua wananchi wa Mtaa wa Sokola Kata ya Majengo iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wamesema wanachukua tahadhari ya  kuziba madinbwi hayo ya  maji.

Wakizungumza na Huheso Fm wamesema hali ya madimbwi katika mtaa wao ipo hivyo kila mtu anatakiwa kuchua hatua kwa kushirikiana na jamii ili kuepusha madhara kwa watoto na watu wazima.

Kwa upande wake Mweneykiti Mtaa wa Sokola Patroba Privatusi amesema wanachukua hatua za kuhamasisha wananchi kuziba madimbwi kupitia wataalamu wa afya kuhakikisha madimbwi na mashimo vyoo hatarishi yanafunikwa.

Hata hivyo wananchi wa mtaa wa sokola wmetakiwa kufukia mashimo hayo kwa hiari yao na watakapokaidi watachukuliwa hatua za kisheria,