Huheso FM

Manispaa ya Kahama wazindua Jukwaa la uwekezaji Wanawake kiuchumi

January 12, 2022, 5:45 pm

Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga limezinduliwa leo lengo likiwa kuwazesha wanawake katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Uzinduzi wa jukwaa hilo la wanawake kiuchumi umefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kahama ambapo mgeni rasmi akiwa katibu tawala wa Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya.

Akisoma taarifa ya uzinduzi wa jukwaa la wanawake, Hilda Robert amesema majukwaa ya wanawake yatasaidia kuongeza uelewa wa masuala ya kiuchumi kwa kuwaongoza watanzania kwenye uchumi imara.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye  uzinduzi wa jukwaa hilo Katibu tawala wa Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya amesema mwanamke akiwezeshwa kiuchumi ataleta manufaa kwenye jamii yake.

Hata hivyo jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Manispaa ya Kahama limechagua viongozi ambao watasimamia shughuli zote za jukwaa hilo.