Huheso FM

Viongozi wa Serikali za Mitaa wapewa maagizo kwenye sekta ya elimu

January 9, 2022, 5:20 pm

Picha ya Mbunge wa jimbo la la Kahama Mjini Jumanne Kishimba akiwa na Viongozi mbalimbali wa Mtaa

Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanasimamia zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wanaotarajia kuanza Elimu ya msingi.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Kahama ambapo amesema kuwa mwanafunzi anaetakiwa kuwa shule ni lazima awe shuleni.

Kishimba amesema mwanafunzi ambaye hana sare za shule ni lazima aende shule ili kumsaidia mwanafunzi huyo kutimiza ndoto zake hata kama hana uwezo.

Sauti ya Mbunge Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba

Kwa upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa wakati wakiwakilisha changamoto zao wamesema changamoto kubwa ni kuwepo kwa maboma ya shule ambayo hayajakamilika kujengwa baadhi ya mitaa.

Sauti za viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji

Mbunge Kishimba kwa kuanza mwaka mpya 2022 ameamua kuwakutanisha wenyeviti wa serikali za mitaa kwa pamoja ili kuweza kujua changamoto zilizopo kwa wananchi waliopo kwenye jimbo lake.