Huheso FM

Wananchi wazungumzia uelewa wa magonjwa yasiyo ambukiza

November 10, 2021, 8:10 pm

Wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamesema magonjwa yasiyoambukizwa yamekuwa ni changamoto kutokana na maisha ya mazoea katika jamii.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema watu wengi wanaopata magonjwa yasiyoambukizwa hawatambui mapema kutokana na kutokuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara.

Kwa upande wake Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Dkt. Flora Mwinuka amesema wananchi wanapaswa kufika vituo vya afya mara kwa mara kuchunguza afya zao.

Hata hivyo amesema maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yameanza tarehe 7 mwezi huu na yanatarajia kufikia tamati tarehe 14 Novemba mwaka huu.