Huheso FM

Usalama wa wanafunzi mashuleni wawapatia changamoto

October 30, 2021, 11:49 pm

Imeelezwa kuwa Usalama wa wanafunzi ndani na nje ya shule imekua changamoto hali inayowapelekea kushuka katika masomo yao katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Wameyasema hayo leo wanafunzi wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ghama Hotel ambapo kimejumuisha shule za Sekondari tatu na msingi mbili kwenye kata tano ikiwemo zongomela,Mondo,Kinaga,Kilago na Ngogwa na kuongozwa na Mratibu wa Mwanamke Amka Joyce Michal

Wakizungumza  wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo wamesema moja ya mazingira nayowakosesha usalama wawapo  shuleni ni ukosefu wa taulo za kike kwa wasichana ambapo hali hiyo inawakosesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Naye mwalimu wa shule ya sekondari Isinuka Mary Jelome amesema wao wanahakikisha wanafunzi shuleni wanaishi mazingira safi kwa watoto wa kike ikiwa kama changamoto hizo zipo ndani ya uwezo wao huzitatua pale pale.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo Kata ya Mondo Anna Tesha amesema wamekua wakifanya mikutano na vikao kwa wadau wa maendeleo na wananchi ili kuibua changamoto za usalama wa wanafunzi mashuleni.

Mradi wa Mwanamke Amka unaolenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto unaratibiwa na Joyce Michael na unafadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS) na unatekelezwa, Kinaga,Ngongwa, Mondo,kilago na kilago zilizopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.