Huheso FM

Wakulima wapewa ruzuku za pembejeo

October 13, 2021, 12:45 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amewataka wakulima waliopatiwa ruzuku za pembejeo za kilimo na halmashauri kuhakikisha wanatumia vizuri pembejeo hizo kwenye kilimo kama ilivyokusudia.

Festo kiswaga ameyasema hayo wakati akigawa  pembejeo hizo kwa wakulima ambapo amesema wakulima waliopatiwa  pembejeo hizo atahakikisha anawafuatilia pindi wanapoanza kulima hadi mavuno ilikuweza kujua ni kiasi gani kimepatikana kupitia mpango huo.

Katika ugawaji huo Mkuu wa Idara ya Kilimo, umwagiliaji na ushirika Manispaa ya kahama, Richard Lazaro amesema mpango huo wa kugawa Ruzuku umeweza kuwasaidia baadhi ya wakulima ambao waliweza kugaiwa mwaka uliopita.

Kwa upande wao wakulima walioweza kugaiwa pembejeo za kilimo wameeleza namna mipango na mikakati waliojiwekea katika kuakikisha wanalima kilimo chenye tija.

Hata hivyo Manispaa ya Kahama ilianzisha utaratibu wa kutoa ruzuku za pembejeo  kwa wakulima vijana kuanzia msimu wa kilimo 2018/2019 kwa kutumia bajeti ya Halmashauri  kupitia mapato ya ndani nz Pembejeo hizo zimenunuliwa kwa milioni 54.