Huheso FM

Mbunge aendelea kuchangia ujenzi wa shule za sekondari

October 1, 2021, 11:26 am

Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga, Jumanne Kishimba amechangia millioni moja laki mbili na elfu hamsini kwa ajili ya ununuzi vifaa vya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Kagongwa.

Akizungumza katika ziara yake aliyoifanya ya kutembelea miradi mbalimbali katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya kagongwa amesema wanatarajia kufikia Januari shule hiyo itakua imemalizika na wanafunzi wataanza kusoma.

Sauti ya Mbunge jimbo la Kahama mjini

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Gembe, Kata ya Kagongwa, Andrea Dosa amesema shule hiyo ikimalizika itawasaidia wanafunzi wote waliokua wanatembea umbali mrefu kwenda shule pia itawajengea ufaulu mzuri katika masomo yao.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Gembe

Naye Mtendaji wa Kata ya Kagongwa, Jerome Lugoma amesema wanatarajia kujenga vyumba 12 vya madarasa maabara moja na Jengo la Utawala na utagharimu millioni 68 ambazo zitamaliza ujenzi huo na itajumuisha michango ya wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.