Huheso FM

Wanaume chanzo cha ukatili wa kijinsia

September 28, 2021, 8:36 pm

Picha za wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia katika Mradi wa Mwanamke Amka

Imeelezwa baadhi ya wanaume ndio chanzo kikubwa cha ukatili wa kijinsia katika jamii kutokana na kutokua tayari kupokea mabadiliko ya kupinga vitendo vya ukatili wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu mradi wa MWANAMKE AMKA Joyce Michael wakati akizungumza kwenye Kikao cha siku moja iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa Ghama hotel wilayani humo.

Amesema wanaume wamekua na mifumo dume ambayo inasababisha mila na desturi kandamizi, kushindwa kubadilika na tamaa ambayo inapelekea vitendo vya ukatili.

Sauti ya Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka Joyce Michael

Kwa upande wao wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani humo wamesema imeonekana wao ndio chanzo kikubwa kinachopelekea ukatili wa kijinsia na kuwepo kwa mifumo dume hivyo elimu iendelee kutolewe mara kwa mara katika jamii.

Sauti za Wadau mbali mbali wa kupinga ukatili wa kijinsia katika Mradi wa Mwanamke Amka

Kwa upande wake afisa maendeleo kata ya Ngogwa, Ester Sanga ameshauri kupanua wigo wa kutoa elimu hususani shule za sekondari na msingi kuwaaalika walimu wa kiume na kuwapa elimu kwa sababu imeonekana mashuleni ndio chanzo cha ukatili wa kijinsia.

Sauti ya afsa maendeleo Kata ya Ngongwa Ester Sanga

Warsha hiyo ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia imehusisha madereva pikipiki maarufu bodaboda,wananchi wa kawaida, viongozi wa serikali za mitaa na wadau mbalimbali wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga

Picha ya Mratibu wa Mradi wa Mwanmke Amka Joyce Michael