Huheso FM

Wananchi watakiwa kujitokeza ujenzi wa Bomba la Mafuta-Kahama

September 22, 2021, 4:49 pm

picha ya wadau wa EWURA waliohudhuria kikao

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amewataka wananchi wilayani humo kuchangamkia fursa za mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ambao unapita wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa EWURA na TPDC ambacho kimeshirikisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Wilaya ya Kahama mkuu wa Wilaya huyo amesema atahakikisha anawasaidia wanakahama kupata fursa hizo ili waweze kunufaika na mradi huo.

Amesema dhamira yake ni  kuona wafanyabiashara wilayani humo wanapata tenda hizo na kuwaomba wale wote watakaopata tenda hizo kuacha ubabaishaji wafanye kazi kwa weledi ili kujenga uaminifu zaidi.

sauti ya mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga

Kwa upande wao wawezeshaji kutoka EWURA na TPDC wamesema dhamira ya kikao hicho ni kuhakikisha wazawa wanashiriki katika mradi huo wa Bomba la mafuta kwa sababu unapita katika eneo lao.

Hata hivyo mradi  huo wa Bomba la mafuta utajengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka  mkoani Tanga nchini Tanzania.