Huheso FM

Jeshi la Zimamoto latumia gari moja kuhudumia halmashauri tatu

September 22, 2021, 3:18 pm

Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani Kahama mkoani Shinyanga limesema linakabiliwa na uhaba wa vifaa vya uokozi ikiwemo Magari.

Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi hilo Hanafi Mkilindi wakati akizungumza na Huheso fm redio kuhusu mikakati ambayo wamekuwa wakiifanya katika majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza.

 Amesema jeshi la Zimamoto katika Wilaya ya Kahama licha ya kuwa na vifaa vichache vya uokoaji pia miundombinu ya barabara nayo imekuwa changamoto kufika kwa wakati eneo la tukio.

sauti ya Kamanda wa jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani Kahama, Hanafi Mkilindi

Hata hivyo jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Kahama mkoani Shinyanga linahudumia halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama mji ambapo linatumia gari moja pekee katika matukio yanayojitokeza.