Huheso FM

Vikundi vyapewa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

September 20, 2021, 3:16 pm

Wajumbe wa Mradi wa Mwanamke Amka

Wajumbe wa mradi wa mwanamke amka unaolenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto waliopo mashuleni Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia kwenye vikundi vyao.

Hayo yamesemwa na mratibu wa mradi wa mwanamke amka, Joyce Michael katika warsha iliyofanyikia kwenye ukumbi wa Ghamma hotel ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kupinga, kuepukana na kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Amesema kila mmoja awe tayari kupokea elimu kutoka sehemu tofauti tofauti na kuwa balozi kwa mtu mwingine katika kupinga ukatili wa kijinsia kwenye jamii inayomzunguka.

Sauti ya Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka

Nao wajumbe wa mradi wa MWANAMKE AMKA wanaotoka katika kata tofauti tofauti katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamesema kutokana na mafunzo hayo waliyoyapata watakwenda kutoa elimu kwenye vikundi vyao na jamii kwa ujumla.

Sauti za wajumbe wa Mradi wa Mwanamke Amka

Mradi wa MWANAMKE AMKA unaolenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto unafadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS) na unatekelezwa na shirika la HUHESO Foundation katika Kata tano za  Zongomela, Kinaga, Ngongwa, Mondo, na Kilago zilizopo Manispaa ya kahama.

PIicha ya Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka