Huheso FM

Baiskeli 40 kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya Ukimwi

July 26, 2021, 6:46 pm

picha ya mabinti wawezeshaji

Mabinti wenye umri kati ya miaka 15-24 wa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wamepatiwa Baiskeli zaidi ya 36 kwa ajili ya uelimishaji rika juu ya kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Baiskeli hizo zimetolewa na shirika la Huheso Foundation kwa kushirikiana na shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ajili ya kuwawezesha mabinti hao katika usafiri ili kuyafikia makundi mbalimbali ya mabinti ili kutoa elimu ya kupima afya zao.

Akizungumza katika zoezi la kukabidhi baiskeli hizo afisa mradi wa EPIC, David Edson amesema baiskeli hizo ni maalum kwa mabinti hao ambao ni wawezeshaji kusafiri katika kila Kata ili kutoa elimu ya kupima maambukizi ya ukimwi, Elimu ya uchumi na mikopo.

sauti ya afisa mradi EPIC, David Edson

Hata hivyo afisa mradi huyo amesema wanatarajia kuona manufaa makubwa ya mabinti kujisimamia baada ya kupatiwa elimu kupitia mabinti hao waliopatiwa baiskeli lengo kubwa ni kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi.