Huheso FM

Jambazi kutoka Dar es salaam auawa Shinyanga

May 31, 2021, 5:44 pm

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Idd Masasi (43) anayedaiwa kuwa Jambazi ameuawa baada ya kupigwa risasi mguuni na mgongoni na askari polisi na alifariki wakati akipatiwa matibabu hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema Jeshi la polisi lilipata za uwepo wa Jambazi huyo mkazi wa Ndembezi Mjini Shinyanga na makazi mengine Kigamboni Jijini Dar es salaam.

Kamanda Magiligimba Amesema kumbukumbu zinaonesha kuwa Idd Masasi alishawahi kuhukumiwa kufungwa miaka 30 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2011 na kutumikia adhabu hiyo katika gereza la Butimba Mwanza na baadae alitoka kwa rufaa.

sauti ya kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba

Hata hivyo kamanda Magiligimba ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Mkoa wa Shinyanga uendelee kuwa salama.

MWISHO