Huheso FM

Wasio na taaluma ya Habari watajwa kuharibu tasnia hiyo Kahama.

May 4, 2021, 3:42 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Anamringi Macha amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanawaondoa waandishi wa habari wasiokuwa na taaluma hiyo ambao wamekuwa wakiharibu tasnia hiyo kwa kuandika habari za uongo.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga  yamefanyika katika Manispaa ya Kahama yakiongozwa na kauli mbiu ni ‘Habari kwa Manufaa ya Umma’ yaliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Macha amewasisitiza waandishi wa habari kuandika habari sahihi kwa manufaa ya umma huku akisema katika wandishi wa habari kuna wandishi wasiokuwa na taaluma wapo kwa maslahi binafsi hivyo wamekuwa wakitishia watu wakitaka fedha na kuharibu sura ya taaluma hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama

Hata hivyo amezitaka taasisi za umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari zitambue vyombo vya habari vilivyopo katika maeneo yao kutoa taarifa mbalimbali na kuepusha waandishi wa habari kuandika taarifa zisizo sahihi.