Huheso FM

Wakulima wa mazao ya nafaka manispaa ya Kahama watakiwa kuvuna mazao yaliokomaa

April 30, 2021, 11:13 am

Wakulima wa mazao ya nafaka katika halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuvuna mazao yao yakiwa yamekomaa na kukauka ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kilimo wa Manispaa ya Kahama Samson Sumuni ambaye amesema wakulima wanatakiwa kuhakikisha mazao yao yanakuwa yamekauka vizuri kabla ya kuyavuna kwani kuyavuna yakiwa hayajakauka vizuri hutengeneza ugonjwa wa sumu kuvu.

Sumuni amesema ugonjwa wa Sumu kuvu husababishwa na ubichi wa mazao kwa kutokukauka vizuri sambamba na kuhifadhiwa sehemu yenye unyevu nyevu hivyo wakati huu wa mavuno wakulima wanapaswa kujiridhisha kama mazao yao yamekauka vizuri.

Sauti ya Afsa kilimo manispaa ya Kahama

Aidha afisa Kilimo Samson Sumuni amesema kuwa mkulima endapo atafuata utaratibu wa kilimo bora kwa kuzingatia upandaji wa mbegu bora  na viuatilifu sahihi  anaweza kuvuna mazao mengi na kunufaika kupitia kilimo.

Sauti ya Afsa kilimo Samson Sumuni

Hata hivyo ugonjwa wa sumu kuvu ni ugonjwa unaopatikana kwenye mazao ya nafaka kama Mahindi, Mpunga na  Karanga endapo mazao hayo yakifadhiwa bila kukauka vizuri au kuhifadhiwa sehemu yenye unyevu unyevu wa maji hukumbwa na ugonjwa huo.