Huheso FM

Wananchi walalamikia miundombinu mibovu ya barabara kwa kukwamisha shughuli zao.

April 28, 2021, 5:33 pm

Wananchi wa Mtaa  wa Inyanga Kata ya Nyihogo halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuwatengenezea barabara ya kutoka Mhungula  kwenda mwime ambayo imeharibika kwa kiwango kikubwa na kuwa changamoto kwao.

Wakizungumza wananchi  hao wamesema suala la miundombinu kwao limekuwa ni changamoto hasa katika kipindi cha masika  jambo ambalo linapelekea kutumia muda mrefu katika usafirishaji wa mizigo pamoja na shughuli zingine za kimaendeleo.

Wamesema changamoto ya barabara imekuwa changamoto ya muda mrefu huku wakiwatupia lawama viongozi wa Kata hiyo hiyo kushindwa kuwasilisha changamoto zao katika mamlaka zinazohusika.

SAUTI ZA WANANCHI

Kwa upande wake meneja wa TARURA Manispaa ya Kahama, Joab Mtagwaba amesema barabara zote zimewekewa wakandarasi ikiwemo ya Mwime hivyo muda wowote kuanzia sasa ukarabati wa barabara hizo utaanza mara moja.

SAUTI MENEJA WA TARURA MANISPAA YA KAHAMA

Hata hivyo meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA, Joab Mtagwaba amewataka wananchi kwa kipindi hiki kuwa wavumilivu huku akiwaomba kutoa ushirikiano kwa wakandarasi kwa wananchi wa maeneo husika pindi ukarabati utakapoanza.

MWISHO