Huheso FM

Wafanyabiashara Kazaroho Manispaa ya Kahama wamuomba Mkurugenzi kuvunja masoko.

April 28, 2021, 5:23 pm

Wafanyabiashara wa soko la Kazaroho wamuomba mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya soko pamoja na kuyaua masoko yaliyopo pembezoni mwa soko hilo yasiyo rasmi.

Wakizungumza baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wamesema awali walitolewa katika soko hilo ili kupisha ukarabati wake na baadae kurudishwa huku baadhi ya muindombinu kama vyoo na barabara bado havijakamilika.

Wafanyabiashara hao pia wamemuomba mkurugenzi kuyavunja masoko ambayo siyo rasmi yaliyopembeni kwani yanaua mitaji yao kwa wateja kushindwa kununua bidhaa ikizingatiwa wao wanalipia kodi ya pango la kufanyia biashara.

SAUTI ZA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KAZAROHO

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba amesema awali alikubaliana na uongozi wa soko uliopita kuwa wajenge vyoo na kusimamia ili kupata mapato badala yake walishindwa kutekeleza hivyo vyoo hivyo vitajengwa na halmashauri.

SAUTI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA KAHAMA

Hata hivyo Soko hilo lipo katika Kata ya Nyihogo ambalo wafanyabiashara hao mwaka uliopita waliondolewa ili kupisha ukarabati wake hivyo kwa sasa wamerejea ndani ya soko hilo kufanya biashara zao.

MWISHO