Huheso FM

RPC Shinyanga “Madereva tumieni hekima kuendesha magari yenu”

April 26, 2021, 5:04 pm

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba amefanya ukaguzi wa kushtukiza kwa mabasi yaendayo mikoani kutoka Kituo Cha Mabasi Kahama mkoani humo.

Akizungumza na madereva  na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria kamanda Magiligimba amesema magari yote yaendayo mikoani kuhakikisha wanakuwa madereva wawili ili kujilinda na ajali zisizotarajiwa huku akiwataka kuacha kwa kuendesha kwa mwendokasi.

Kamanda Magiligimba pia amewataka abiria wote wanaosafiri kuhakikisha wanatoa taarifa za mwendokasi na vihatarishi ambavyo vinafanywa na dereva wa gari husika ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka ili kudhibiti ajali za barabarani.

SAUTI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA

Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga alifanya ukaguzi huo wa kushtukiza katika kituo cha mabasi Kahama April 25, 2021 majira ya saa kumi na moja alfajiri kwa lengo la kutoa elimu kwa abiria pamoja na ukaguzi wa mabasi.

MWISHO