Huheso FM

Miundo mbinu ya barabara yawa changamoto kwa wananchi

April 20, 2021, 12:18 pm

Wananchi wa Mtaa wa Malunga Kata ya Malunga  iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara katika maeneo yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na HUHESO FM wananchi wa Mtaa huo wamesema changamoto ya miundombinu ya barabara imekuwa kikwazo kwao kutokana na barabara kutokuwa rafiki katika shughuli zao kwani hazipitiki kwa ur

Sauti za wananchi wa kata ya Malunga

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Malunga, Omary Abdallah amesema halmshauri imepanga bajeti ya fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hizo na mkandarasi tayari ameshaanza kazi baadhi ya maeneo katika Kata hiyo.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Malunga Kata ya Malunga

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Malunga, Joseph Mipiwa amesema fedha za ujenzi wa barabara zimeshatolewa na kinachosubiri ni Mvua zitakapoacha kunyesha ukarabati wa barabara hizo utaanza rasmi.

Picha ya barabara ya mtaa wa Malunga