Huheso FM

Manispaa ya Kahama yaanza utoaji wa hati ya Ardhi

April 12, 2021, 5:05 pm

Kufuatia tamko la waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi kuwataka wananchi kupima viwanja na kila mwenye kiwanja kumiliki hati ya Ardhi wananchi katika Manispaa ya Kahama wametakiwa kujitokeza kuchukua hati zao kwa wale waliolipia.

Kauli hiyo imetolewa na Usila Mtatifikolo ambae ni  afisa Ardhi mteule wa Manispaa ya Kahama wakati akizungumza na Huheso fm ofisini kwake amesema zoezi hilo la utoaji hati litaanza April 12 katika ofisi za Ardhi mjini humo.

Mtatifikolo amesema zoezi hilo la kuchukua hati ili kuepusha usumbufu wananchi na wakazi wa Manispaa ya Kahama wasichukuliane hati hizo bali mhusika wa hati ya ardhi kwenda kuchukua.

Hata hivyo zoezi hilo linatarajia kuwa la siku tano ambalo limeanza leo jumatatu April 12 hadi Ijumaa April 16 mwaka huu.