Huheso FM

Mwalimu awalazimisha wanafunzi kuzoa kinyesi cha binadamu kwa mikono Kahama.

March 30, 2021, 11:49 am

Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Kayenze iliyopo kata ya Ukune halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga anadaiwa kutoa adhabu kwa wanafunzi wanne kuzoa kinyesi kwa kutumia mikono.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kayenze, Thomas Magandula amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea mwezi uliopita wa Februari mwaka huu ambapo wanafunzi hao walikuwa wanne kati yao watatu waliinamishwa kwenye tundu la choo na mmoja kushika kinyesi.

Magandula amesema majina ya wanafunzi hao ameyahifadhi na amefuatilia tukio hilo namna lilivyotokea ambapo mwanafunzi alielazimishwa kushika kinyesi alituhumiwa kumtaka kimapenzi mwanafunzi mwenzake ambaye ni mtoto wa mwalimu wa shule hiyo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kayenze, Thomas Magandula

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo Jumanne Punguja amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akithibitisha kuwa tayari kikao cha wazazi wa wanafunzi pamoja na kamati ya shule umekaa na kuzungumzia suala hilo lakini halina ukweli kama inavyoelezwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Jumanne Punguja

Hata hivyo Mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni katibu wa kamati ya shule amesema tukio hilo halijatokea shuleni kwake huku akisema hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.