Huheso FM

Nec yatangaza uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe Kigoma.

March 28, 2021, 11:26 am

Nec yatangaza uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe Kigoma.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Muhambwe, mkoani Kigoma baada ya kupokea Barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi.

Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari Jijini Dodoma leo, 27 Machi, 2021, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera amesema uchaguzi huo umeapangwa kufanyika tarehe 2 Mei,2021.

Alisema kuwa maandalizi kwaajili ya uchaguzi huo yameshafanyika na kazi ya utoaji fomu za uchaguzi kwa wagombea inaanza 28 Machi hadi 3 Aprili, 2021 huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hiyo ukifanyika 3 Aprili mwaka huu.
Aidha Dkt Mahera amesema kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo zitaanza 3 Aprili 2021 na zitafikia ukomo wake Mei mosi mwaka huu na uchaguzi kufanyika 2 Mei,2021.

Mahera alisema yayari Tume imekwisha vitaarifu Vyama vya Siasa kwa njia ya barua juu ya kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo na inavikumbusha kuzingatia sharia, kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Miongozona Maelekezo ya Tume wakati wote wa kipindi cha Uchaguzi.

Pia Mahera alitumia fursa hiyo kutoa salamu za pole kwa viongozi wa Serikali, Familia na Watanzania wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli.