Highlands FM

Vijana mkoani Mbeya wapewa mbinu za kujikwamua kiuchumi

15 September 2023, 18:21

Mratibu wa miradi kutoka Ujerumani Mariam Abraham akitoa elimu kwa vijana Mkoani Mbeya :Picha na #Samwel Mpogole

Mafunzo ya uelimishaji rika kwa vijana yatasaidia kuondoa changamoto katika masuala ya afya na uchumi.

Na mwandhisi wetu Samwel Mpogole

Vijana wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo ya uelimishaji rika kwa lengo la kusaidia vijana wengine waliopo kwenye jamii kuepukana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na maswala ya afya na Uchumi.

Hayo yameelezwa na Mariam Abraham mratibu wa mradi wa maendeleo kwa vijana ulio ndani ya shirika la  DSW walipofika katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini kata ya Utengule Usongwe walipokuwa wakitambulisha mradi wavijana wa shirika hilo

Kwaupande wao vijana waliofika katika semina hiyo wamewashukuru wawezeshaji kutoka shirika Hilo kwa kutambua thamani yao vijana hao na kuahidi kuwanao bega kwa bega katika kufanikisha Marengo ya shirika hilo

Mratibu wa miradi kutoka Ujerumani Mariam Abraham akitoa elimu kwa vijana Mkoani Mbeya :Picha na #Samwel Mpogole