Wenye ulemavu watakiwa kutambua afya ya akili
10 December 2024, 5:08 pm
Miongoni mwa msaada uliotolewa na taasisi ya Tfed ni pamoja na majiko ya gesi, fimbo nyeupe, cherehani, kiti mwendo na mafuta kwa watu wenye ualbino.
Na Yussuph Hassan.
Imeelezwa kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa kundi la watu wenye ulemavu kutambua afya ya akili ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Foundation for Excellence in Disabilities wakati taasisi hiyo ilipokutana na kundi la watu wenye ulemavu pamoja Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa msaada ya elimu ya uchunguzi na utambuzi wa afya ya akili.
Kwa upande wake Isaack Mwamakula mtaalam kutoka taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela hapa anabainisha kwanini wamelenga kundi la watu wenye ulemavu kwa ajili ya kufanya uchunguzi na utambuzi wa afya ya akili.
Kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Katibu Shiviwata walaya ya Dodoma amewataka washiriki hao kutoa ushirikiano katika mafunzo hayo.
Taasisi ya Tanzania Foundation for Excellence and Disabilities Tfed imeendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya nishati safi.