Dodoma FM

Kulaya: Bado tunaangazia miswada ya sheria iliyowasilishwa bungeni

20 November 2023, 7:38 pm

Moja ya mapendekezo yao ni kuona sheria hiyo inafafanua vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ukatili dhidi ya Wanawake  wakati wa Uchaguzi.Picha na WILDAF.

Kumbuka kuwa miswada hiyo ni pamoja na wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023, muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023.

Na Seleman Kodima.

Na leo tunapata maoni ya Mkurugenzi Mkuu wa WilDAF, Anna Kulaya amesema iwapo maboresho hayo yatafanikiwa kama mapendekezo ya wadau yanavyoangazia Sheria hizo tatu itasaidia ushiriki mkubwa wa wanawake katika ngazi za Maamuzi na Siasa.

Akizungumzia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,Kulaya amesema moja ya mapendekezo yao ni kuona sheria hiyo inafafanua Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia hususani Ukatili dhidi ya Wanawake  wakati wa Uchaguzi.

Amesema na hatua hiyo ianze ndani ya Vyama vya Siasa hadi katika hatua zote za Uchaguzi na itoe mbiu mbalimbali za kukabiliana na Vitendo hivyo ili kuruhusu wanawake wengi washiriki katika masuala ya Uchaguzi.