Dodoma FM

Shekimweri ataka ofisi ya mtaa wa kwa Mathias Miyuji kuwa ya mfano

19 September 2023, 3:43 pm

Picha ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabiri Shekimweri akikagua ujenzi wa ofisi hiyo. Picha na David Kavindi.

Ujenzi wa jengo la ofisi ya mtaa wa mathias jijini dodoma unaosimamiwa na kampuni ya urasimishaji ardhi ya wise plan unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.

Na David Kavindi.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ameiagiza kampuni ya wise plan limited kuhakikisha inakamilisha kwa wakati ujenzi wa ofisi ya Mtaa wa Mathias uliopo Kata ya Miyuji Jijini Dodoma

Ameyasema hayo wakati wa akikagua ujenzi wa ofisi ya mtaa wa mathias ambapo amesema kuwa ofisi hiyo inapaswa kuwa ya mfano katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Mh. Shekimweri.

Shekimweri amesema serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu imetoa fedha kiasi cha shilingi millioni tano kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa ofisi hiyo.

Sauti ya Mh. Shekimweri.
Picha ni mkurugenzi wa kampuni ya wise plan Antpas mtui ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa ofisi hiyo. Picha na David Kavindi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya wise plan Antpas mtui ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa ofisi hiyo amesema kiasi cha shilingi millioni kumi na mbili zimeshatumika katika ujenzi wa ofisi hiyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa wise.