Dodoma FM

Mapinduzi A waomba nyumba ya daktari wa zahati yao

19 September 2023, 5:01 pm

Picha ni wakazi wa eneo hilo wakizungumza na Dodoma fm Radio.Picha na Dodoma fm.

Hata hivyo Serikali inawataka wawekezaji wote nchini kushiriki kikamilifu  katika kutatua  changamoto zinazo  wakabili wananchi walio karibu na mradi wa mwekezaji huyo.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa mtaa wa mpinduzi A wameiomba Serikali na wadau wa afya kuwasaidia kupatikana wa nyumba ya mganga wa zahanati yao ili kuwa uhakika wa kupata huduma.

Wameeleza kuwa kukosekana kwa nyumba za watumishi katika eneo hilo inapelekea watumishi hao kurudi kwenye makazi yao ambayo yapo mbali na eneo lao la kazi hivyo kusababisha baadhi ya watu kukosa huduma.

Aidha wameongeza kuwa ni vyema Serikali Kuweka mkazo wa nyumba za watumishi hususani wa afya ili iwe rahisi kukabiliana na matukio ya dharula katika zahanati zao

Sauti za Wananchi.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Philimoni Makali amesema kuwa licha ya upatikanaji wa madawa katika zahanati hiyo lakini changamoto imekuwa ni kukosekana kwa nyumba za watumishi

Sauti ya Bw. Philipo Makali.

Makali ameongeza kuwa wamejaribu kuomba msaada kwa mwekezaji wa kusaga kokoto kijijini hapo ambapo hawakufanikiwa lakini mwekezaji huyo amewaahidi  baada ya kumaliza ukarabati wa ofisi ataanza ujenzi wa nyumba ya mganga

Sauti ya Bw. Philipo Makali.